Zanzibar: Asilimia 27.4 ya Vijana hawana ajira

0
21

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali imesema idadi ya vijana wasiokuwa na ajira imefikia 109,868 sawa na asilimia 27.4.

Akitoa ufafanuzi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mudrik Ramadhan Soraga amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira ikiwemo kuibua miradi ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na fedha za UVIKO19, shilingi bilioni 36 ambazo zimetengwa kwa ajili ya kuyawezesha makundi ikiwemo vijana kujiajiri pamoja na vijana waliojikita katika ujasiriamali wa kuzalisha mazao ya baharini ikiwemo ufugaji wa samaki, majongoo ya baharini na kaa.

Ameongeza kuwa Serikali imeanza kujenga vituo vikubwa kwa ajili ya kuzalisha ajira kwa vijana kupitia kazi mbalimbali ikiwemo kazi za mikono za uzalishaji.

Send this to a friend