Zanzibar kulegeza masharti ya kudhibiti corona

0
39

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein amesema serikali visiwani humo inakusudia kulegeza masharti  yaliyowekwa katika kupambana na maradhi ya virusi vya Corona wakati wowote kuanzia sasa.

Rais Shein ametoa kauli hiyo na kuongeza kuwa hali ya sasa ni nzuri ambapo Zanzibar ina wagonjwa 34 tu.

“Uamuzi wa kuelegeza mashrti hayo kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utatolewa muda wowote kuanzia sasa,” amesema Dkt Shein.

Kwa mara ya kwanza waumini wa dini ya Kiislamu jana walisherehekea sikukuu ya Eid ul Fitr kwa namna ya tofauti ambapo hakukuwa na shamra shamra zilizozoeleka kutokana na uwepo wa ugonjwa wa corona.

Send this to a friend