Serikali Zanzibar: Kuna ongezeko la watoto wahamiaji holela kutoka Bara

0
98

Serikali ya Zanzibar imesema kuna ongezeko la uhamiaji holela wa watoto kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar unaochangiwa na umaskini na unyanyasaji.

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar, Abeida Rashid ametoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo ya kitaifa ya kushughulikia uhamiaji haramu na kuimarisha ulinzi wa wahamiaji wanaoishi katika mazingira hatarishi Tanzania.

Amesema mwaka jana watoto 66 waligunduliwa mitaani baada ya kuingia Zanzibar kwa njia zisizo halali kutoka Tanzania Bara.

“Kuanzia Januari hadi mwezi huu, tuliwakuta 19 ambao wamepelekwa kwenye nyumba salama ambako wanapata mafunzo muhimu ili kujikimu,” amesema.

Chanzo: The Citizen Tanzania