Zanzibar kupiga marufuku shisha na sigara za kielektroniki

0
63

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepanga kupiga marufuku uagizaji na utumiaji wa Shisha na E-sigara ikidai kuwa inatumika hovyo katika maeneo mbalimbali ya umma.

Katika mahojiano na vyombo vya habari, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa Zanzibar, Masoud Ali Mohammed amesema serikali itatoa agizo maalum hivi karibuni.

“Sote ni mashahidi, unywaji wa Shisha na E-sigara umekuwa jambo la kawaida, na tutakuja na sheria maalum ya udhibiti ili kuwasimamia wale ambao watakuwa na vibali maalum vya kuagiza na kuuza shisha au sigara hizo,” amesema Masoud.

Utafiti mpya: Unywaji pombe wa wastani hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo

Aidha, Waziri Masoud amewataka waagizaji wa bidhaa hizo kusitisha kuagiza bidhaa kwani watalazimika kufuata sheria mpya ambayo serikali itatoa.

Kwa mujibu wa ripoti ya The Citizen, baadhi ya wafanyabiashara wa mahoteli Zanzibar wamedai shisha ni maarufu sana katika hoteli za kitalii na migahawa, hivyo kupigwa marufuku kwa bidhaa hiyo kunaweza kusababisha hasara kubwa katika upande wa mapato.

Send this to a friend