Zanzibar yakanusha kuwepo muathirika wa Corona

0
43

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa muathirika wa virusi vya Corona katika Hospitali ya Global visiwani humo.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar, Dkt. Juma Mohammed Salum amesema kuwa taarifa hizo zinasambazwa na watu wasioitakia mema Zanzibar ili kusababisha taharuki kwa jamii kwa lengo wanalolijua wao.

Dkt. Salum amewataka wananchi kupuuza taarifa hizo za uongo na kusikiliza taarifa rasmi zinazotolewa na serikali.

Aidha, serikali imesema inawafuatilia kwa karibu wale walioeneza taarifa hizo na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ili iwe funzo kwa wengine.

Taarifa hizo zilianza kusambaa baada ya watu wawili, raia wa Ujerumani na Ghana waliowasili Zanzibar wiki moja iliyopita kufika hospitalini hapo Machi 17, 2020 kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya homa, mafua, na kikohozi.

Hadi hivi sasa hakuna mtu aliyegundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona visiwani Zanzibar, na wananchi wameaswa kuchukua tahadhari badala ya kukimbilia tatizo.

Send this to a friend