Zanzibar yapiga marufuku kupiga muziki viwanja vya sikukuu

0
44

Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Unguja Kisiwani Zanzibar imepiga marufuku upigaji wa muziki katika viwanja mbalimbali vya kusheherekea sikukuu ya Eid-el-fitri.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkuu wa Mkoa Ayoub Muhamed Mahmoud amesema kuwa ni marufuku kupiga muziki katika viwanja vya wazi katika kusheherekea  sikukuu hiyo.

Aidha amewataka wamiliki wa mahoteli ya kitalii ambao wana kumbi za starehe kuhakikisha wanafuata masharti yaliyowekwa na serikali ya mkoa huo.

Hata hivyo Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Elisante Makiko Mmary amesema Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wote watakaokiuka sheria zilizowekwa ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wazazi na walezi watakaowaacha Watoto kwenda kwenye viwanja peke yao bila uangalizi.

Send this to a friend