Zanzibar yazindua teknolojia ya kupima UVIKO19 kwa haraka zaidi

0
39

Zanzibar imeingia kwenye historia ya kuwa nchi ya kwanza Afrika kuzindua teknolojia mpya ya haraka ya upimaji wa Virusi vya UVIKO19, itakayoweza kutambua chembe chembe za maambukizi kwa dakika chache, tofauti na vipimo vingine ambavyo vinavyotumika barani Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amesema teknolojia hiyo itawapa unafuu na itawaondolea usumbufu wasafiri na watalii wanaoitembelea Zanzibar.

Aidha, amesema tayari wamefanya makubaliano na kampuni ya Sunmade ya Abu Dhabi kuleta mashine maalum ya EDE Scan ambayo itawasaidia watu kufanya vipimo hivyo na kupata majibu ndani ya muda mchache.

Awali, wasafiri walilazimika kutumia saa 24 kupata majibu ya vipimo vya UVIKO19 kabla ya kusafiri uwanja wa ndege. Kupitia kipimo hicho, sasa itachukua saa moja hadi mbili kupata majibu yao kabla ya kusafiri.

Hata hivyo mazungumzo kati ya Tanzania Bara na Zanzibar yanaendelea ili kuangalia uwezekano wa teknolojia hiyo kuanza kutumika pande zote mbili.

 

Send this to a friend