ZBC yaomba radhi kwa tamthilia iliyoonesha wapenzi wakiwa kitandani

0
38

Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) limeomba radhi kufuatia kipindi cha tamthliya ya Fundisho kilichorushwa kupitia ZBC TV jana Februari 15, 2023 saa nne usiku kwenda kinyume na maadili.

Kipande hicho (scene) cha video kilichoruka kilionesha wapenzi wakiwa kitandani, maudhui ambayo yamedaiwa kwenda kinyume na maadili ya taaluma ya tasnia ya habari.

Tamthliya hiyo ilionesha ‘scene’ inayomuonesha mwanamke aliyeigiza akiwa amevalia kanga moja kitandani huku mwanaume akiwa amevaa bukta pekee.

ZBC imeomba radhi baada ya picha mbalimbali zilizopigwa na kusambazwa mitandaoni na wengine wakilalamika kuhusu maudhui yake kukosa maadili yanayoendana na Zanzibar.

Send this to a friend