Ziara ya Rais Samia Korea Kusini yafanikisha mradi wa majitaka Dar es Salaam

0
23

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema ziara iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan nchini Korea Kusini imetengeneza mahusiano mazuri na kuchangia kupatikana kwa fedha kwa ajili ya miradi mikubwa ya maji safi na usafi wa mazingira.

Ameyasema hayo leo Desemba 16, 2024 baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Mfumo wa Kutibu Majitaka Katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni siku chache baada ya ziara ya Waziri Aweso na timu nzima ya sekta ya Maji Nchini Korea Kusini.

“Baada ya kupata nafasi ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya ziara ya Korea Kusini kwa muda mfupi sana, baada ya kumaliza na mimi nimepata nafasi hivi karibuni kwenda haijafika hata wiki tumepata zaidi ya dola za kimarekani zaidi ya milioni 240 kwa ajili ya uwekezaji kwenye maji taka”

Ameongeza kuwa hiyo inathibitisha mahusiano mazuri na urafiki wa thamani uliopo baina ya nchi hizo mbili ikichangiwa na ziara ya Rais Samia nchini humo pamoja na yeye mwenyewe ” sio jambo jepesi kwenda na muda mfupi huo huo ukapata pesa, hii ni kazi kubwa ni kazi nzuri ya mahusiano na kujitoa kwake Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan”

Mradi huo utagharimu zaidi ya dola milioni 90 sawa na bilioni 170 mpaka utakapokamilika ambapo Waziri Aweso amesema itakuwa suluhisho kubwa kwa changamoto za maji na utaongeza wigo wa upatikanaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kutoka asilimia 45 ya sasa hadi asilimia 65.

 

 

 

 

 

Send this to a friend