Ziara ya Rais Samia Marekani yavutia uwekezaji wa trilioni 11

0
25

Rais Samia Suluhu ameshuhudia utiaji saini wa mikataba saba kati ya makampuni ya Marekani na Tanzania, yenye thamani ya TZS trilioni 11.7.

Uwekezaji huo ambao utafanyika nchini Tanzania unatarajiwa kutengeneza jumla ya ajira 301,110 kwenye kilimo, utalii, biashara na sekta nyingine za uchumi.

Rais Samia ameshuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano (MoU), barua za kuonesha nia (letters of intent) na kuanza kwa mazungumzo ya uwekezaji na biashara kati ya makampuni ya nchi hizo mbili.

Miradi mingine iliyotiwa saini inalenga kuwekeza kwenye mnyororo wa thamani katika kanda ya Kaskazini ya sekta ya utalii wa Tanzania, ikiwemo kwenye maeneo ya kutangaza utalii na kuongeza idadi na ubora wa huduma zinazotolewa.

Rais Samia pia ameshuhudia makampuni ya Marekani yakitangaza nia na mipango ya kuongeza mahusiano yao na Tanzania kwenye maeneo ya uwekezaji na biashara. Makampuni hayo ni pamoja na Upepo Energy, Astra Energy, Crane Currency na Parallel Wireless.

Send this to a friend