Ziara ya Rais Samia nchini India kuwezesha ujenzi wa kiwanda cha simu nchini

0
49

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini India inatarajia kuleta mapinduzi makubwa nchini katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuimarisha sekta za kimkakati pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Makamba amesema ziara hiyo inatarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 8 hadi 11 mwaka huu kwa mwaliko wa viongozi wa India ikiwa ni baada ya miaka minane tangu kiongozi kutoka Tanzania kutembelea nchi hiyo.

Waziri Makamba amesema madhumuni mengine ya ziara hiyo ni kutafuta fursa za biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na India, nchi ambayo inajulikana kwa uchumi mkubwa.

“Kama unavyofahamu, nchi yetu sisi inatafuta maendeleo na moja ya chanzo cha maendeleo ni biashara na uwekezaji na India ni nchi kubwa yenye mtaji mkubwa. Kwahiyo Mheshimiwa Rais anachoenda kufanya pia ni kwenda kuongeza ushawishi ili wawekezaji na wafanyabiashara kutoka India waje kuwekeza hapa nchini. Lakini pia kuendeleza na kukuza biashara inayokuwa kwa kasi kati ya nchi zetu mbili,” amesema.

Kardinali Rugambwa ahimiza umoja na mshikamano kwa Watanzania

Aidha, amesema ziara hiyo inakwenda kuleta manufaa mengi nchini ikiwemo Watanzania kupata fursa mbalimbali za mafunzo nchini India, India kujenga viwanda vya kutengeneza simujanja, kiwanda cha kutengeneza chanjo za binadamu na wanyama, kuanzishwa kwa taasisi ya upandikizaji wa figo, kupata masoko ya kwa ajili ya kilimo, kuanzisha karakana ya vyombo vya majini na kadhalika.

Send this to a friend