Ziara ya Rais Samia nchini Oman yapeleka wawezekaji Njombe

0
66

Baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya ziara Oman, Mkoa wa Njombe umepokea uwekezaji wa mabilioni kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kushrikiana na kampuni ya Bacoin inayomilikiwa na familia ya bilionea Sarah Bamatraf na mwanae Murad Bumatraf.

Kwa mujibu wa taarifa, wawekezaji wameomba mkoa wa Njombe kutoa ekari 100,000 ya ardhi ambayo watawekeza viwanda vya nyama, mradi wa farasi na kilimo cha mashamba makubwa ya parachichi pamoja na kutoa ajira kwa mamia ya wananchi.

Ugeni huo umeripoti katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe ukiwa umeambatana na mbunge wa Afrika Mashariki, Fancy Nkuhi ambaye amesema kwamba, hatua hiyo kubwa ni matokeo ya The Royal Tour filamu iliyofanywa na Rais Samia pamoja na jitihada za Serikali katika kutengeneza mazingira Rafiki ya uwekezaji.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Njombe, Judica Omary amesema mkoa uko yatari kutafuta ardhi kwa namna yayote ili wawekezaji wasalie kuwekeza mkoani humo.

Send this to a friend