Zifahamu Kamandi 6 za JWTZ na majukumu yake

0
53

Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilianzishwa Septemba 01, 1964 likiwa na lengo la kulinda uhuru wa nchi na mipaka ya Tanzania ambapo jukumu lake ni pamoja na kulinda Katiba na uhuru wa Tanzania, ulinzi wa mipaka ya Tanzania, kushiriki katika shughuli za ulinzi wa amani kimataifa, kutoa misaada wakati wa maafa na kadhalika.

Kwa ujumla, JWTZ ina kamandi zinazosimamia sehemu mbalimbali za jeshi hilo ambapo kila kamandi ina viongozi wake wanaosimamia operesheni na maamuzi katika eneo husika.

Hizi ni Kamandi za JWTZ na majukumu yake;

1. Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi;
 Kushughulika na utawala na uendeshaji wa vikosi na shule zilizopo chini ya Makao Makuu ya Jeshi.
 Kuhakikisha maelekezo yanayotolewa na Makao Makuu ya Jeshi yanawafikia walengwa na yanatekelezwa.
 Kusimamia mafunzo na utayari wa kivita.
 Kuhakikisha zana na vifaa vinakuwa katika hali nzuri kiutendaji.

2. Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
 Kuwaandaa maafisa na askari wanaoshiriki katika ulinzi wa amani katika mataifa mengine.
 Kulinda na kuimarisha usalama wa mipaka ya nchi kwa kushirikiana na Kamandi ya Anga na Kamandi ya Wanamaji.
 Kukabiliana na maafa pindi yanapotokea na kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa Ulinzi na Usalama wa nchi na mipaka dhidi ya adui.
 Kusimamia Shule za Mafunzo ya Kijeshi.

3. Kamandi ya Jeshi la Anga
 Kutoa ulinzi wa Anga kwa maeneo muhimu ya kitaifa, kisiasa, kiuchumi na kwa wananchi,
 Kutoa ulinzi wa Anga kwa maeneo na vituo muhimu vya kijeshi.
 Kutoa msaada wa kimapigano kwa operesheni za Majeshi ya Nchi Kavu na Wanamaji.
 Kutoa msaada kwa mamlaka za kiraia hasa nyakati za maafa ya kitaifa na kusindikiza ndege za viongozi na kukusanya taarifa za kiusalama.
 Kushiriki katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

4. Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
 Kuhakikisha mipaka yote katika Bahari, Maziwa na Mito mikubwa inakuwa salama wakati wote.
 Kuwapa ulinzi wa kutosha Wananchi wanaoishi kwa kujishughulisha na uvuvi baharini, maziwa na mito mikubwa.

5. Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
 Malezi ya Vijana
 Kuwapa vijana mbinu za kijeshi wawe Jeshi la Akiba,
 Kuwaandaa vijana watakaofaa kujiunga na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
 Kuwaandaa vijana kusaidia katika majanga mbalimbali, mfano mafuriko, moto na ajali mbali mbali.
 Kuandaa vijana katika uzalishaji mali

6. Kamandi ya Jeshi la Akiba
 Jeshi hili liliundwa kwa lengo la kuandaa nguvu ya akiba kwa ajili ya kusaidiana na Jeshi la kudumu (JWTZ) na vyombo vingine vya usalama katika kudumisha Ulinzi na Usalama wa nchi.