Zifahamu nchi ambazo zimeshafuzu Kombe la Dunia 2022

0
44

Mataifa mbalimbali duniani yako vitani viwanjani kuwania nafasi 32 za kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia ambazo zitafanyika nchini Qatar kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 18 mwaka 2022.

Hadi sasa nchi tatu zimeshapata tiketi ya kwenda Qatar lakini moja wapo ni Qatar ambayo imefuzu moja kwa moja kwa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa zaidi duniani katika soka. Nchi hiyo ilifuzu Desemba 2, 2010 baada ya kuidhinishwa kuwa mwenyeji.

Mataifa mengine ni Ujerumani ambayo ilifuzu Oktoba 11, 2021 baada ya kuifunga Macedonia Kaskazini na hivyo kuongoza Kundi J.

Denmark imekuwa timu ya tatu kufuzu baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Austria Oktoba 12 mwaka huu, hivyo kuimarisha nafasi yake kwenye Kundi F.

Hadi Juni 2022, timu zote zitakazoshiriki fainali hizo zitakuwa zimefahamika.

 

Send this to a friend