Zifahamu sababu kuu mbili za video kupunguziwa “views” YouTube
Tangu kuanzishwa kwake siku ya wapendanao (valentine’s day) mwaka 2005, YouTube umekuwa mtandao mashuhuri kwa wasanii, vyombo vya habari, taasisi za elimu na karibu kila mtu duniani hivi sasa kwani video imekuwa sehemu muhimu ya burudani. Kazi nzuri huonekana mapema. YouTube haikudumu sana katika mikono ya walioianzisha kwani ilikuwa bidhaa adimu na ubunifu wa maana, Novemba 2006 ikanunuliwa na kampuni ya Google kwa karibu shilingi za Kitanzania trilioni 4. Kuanzia hapo YouTube ikaanza kufuata sera za Google na sera mojawapo ni kuhakikisha hakuna wizi wa kazi za watu wala udanganyifu.
Views (idadi ya kutazamwa kwa video fulani) ni kipimo muhimu sana unapoongelea ubora wa kazi na hata umaarufu wa mtoa kazi. Lipo swali kubwa kwa watumiaji wa YouTube nchini Tanzania kwamba inakuwaje unakuta kwa mfano mtu ana views milioni 2 halafu baadaye unakuta zimeshuka hadi milioni na laki nane? Hakika hii hutokea. Mfano tangu mwaka 2019 Novemba Swahili Times imekuwa ikitunza orodha ya views kwa channels za wasanii wa muziki nchini Tanzania na kuna wakati tofauti ya jumla ya views zote za channel toka kuanzishwa kwake mwezi huu na mwezi unaofuatia huwa negative, ikimaanisha kwamba kuna views zinapunguzwa.
Je hii hutokeaje? Ziko sababu tatu kwa mujibu wa wataalamu wa teknolojia na namna ambavyo YouTube inafanya kazi:
Sababu ya kwanza ni kwamba YouTube hupitisha programu maalumu kugundua views feki (hizi huwa ni zile ambazo ni chini ya sekunde 10, au views nyingi kutoka anuani moja ya mtandao kwa wakati mmoja, kitu ambacho ni sifa ya fake views kwa kiswahili twaweza kuita watazamaji makanyaboya au watazamaji ambao si watu halisi).
Wakati fulani programu hiyo ya YouTube huweza kunatisha (freeze) namba ya views katika video bila kuongezeka kwa muda wakati inafanya kazi yake ya kuhakiki. Kwa ufupi Youtube huzuia views zote zenye mashaka mpaka itakapojiridhisha kwamba hazina tatizo.
Sababu ya pili ni ile ya kwamba YouTube ina kazi kubwa ya kupokea content na kuchakata data kwa hiyo hutunza video hizo katika kanzidata (server) tofauti. Kukusanya takwimu server zote kwa pamoja na kuweka jumla kuna muda kuna ucheleweshaji (delays) hasa kwa videos maarufu. Hii inaelezea kwa nini unaweza ku-refresh video ukakuta namba ya views ni ile ile haijabadilika.
Sababu ya kwanza ndiyo muhimu zaidi na yenye kuleta mabadiliko makubwa mara nyingi.
Nicheki Twitter kwa @nyamokomayagilo
***
Maoni ya waandishi wa makala Swahili Times si maoni ya Swahili Times. Unaweza kukutumia makala yako kwa mail@swahilitimes.co.tz