Zifahamu timu za soka kongwe zaidi nchini

0
84

Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ilianzishwa mwaka 1963, ikiwa na maana kwamba mwaka huu wa 2021 imetimiza miaka 58 tangu kuanzishwa kwake. Lakini je wajua kwamba kuna timu kongwe nchini kuliko hata umri wa Ligi hiyo.

Hapa chini tumekuorodheshea timu nne zenye umri mkubwa zaidi nchini toka kuanzishwa kwake hadi kufikia Desemba, 2021.

 

4. Mwadui FC

Timu hii iko mkoani Shinyanga na ilianzishwa mwaka 1956 ikiwa na maana mwaka huu imetimiza miaka 65 tangu kuanzishwa kwake.

3. Coastal Union (Wagosi wa Kaya)

Hii iko mkoani Tanga na ilianzishwa mwaka 1948, ikiwa na maana mwaka huu imetimiza miaka 73 tangu ilipoanzishwa.

2. Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi)

Simba ilianzishwa mwaka 1936 ikiitwa Queens, kabla ya kubadili jina baadaye na kuitwa Eagles kisha Dar Es Salaam Sunderland na baadaye kabisa mwaka 1971 ikabadili jina kuitwa Simba. Mwaka huu Simba imetimiza miaka 85.

1. Yanga

Yanga ina historia ya kuwepo tokea mwaka 1910 lakini ilianzishwa rasmi Februari 11 mwaka 1935. Mwaka huu Yanga imetimiza miaka 86.

Send this to a friend