Zijue album 10 za Bongofleva zilizosikilizwa zaidi

0
38

Mwaka 2021 unaelekea mwishoni, mambo mengi yamefanyika, moja wapo likiwa ni wanamuziki wa Tanzania kutoa ablum na EP za muziki.

Mashabiki wa muziki wamekuwa na mapokeo tofauti ya kazi hizo za wasanii na hapa tuataangazi album na EP zilizotoka mwaka huu ambazo zimesikilizwa zaidi katika mtandao wa Audiomack.

Audiomack inafanya kazi na kampuni mbalimbali za muziki duniani ikiwemo Warner Music Group, Sony Music Entertainment na Universal Music Group.

1. Sound From Afrika – Rayvanny (Milioni 12.5)
Album hii ilitoka Februari 1, 2021 ikiwa na nyimbo 23

2. Definition of Love – Mbosso (Milioni 11.5)
Album hii ilitoka Machi 9, 2021 ikiwa na nyimbo 12

3. Only One King – Alikiba (11.4)
Mfalme wa bongofleva alitoa album hii Oktoba 4, 2021 ikiwa na nyimbo 16

4. High School – Harmonize (Milioni 3.5)
Kutoka Konde Music World Wide, album hii iliingia mtaani Novemba 5, 2021 ikiwa na nyimbo 20.

5. Taste (EP) – Nandy (Milioni 2.7)
Hii ni EP yake ya pili kwa mwaka huu ambapo ya kwanza ni Wanibariki. Taste EP ilitoka Juni 18, 2021 ikiwa na nyimbo nne.

6. Promise (EP) – Lavalava (Milioni 1.8)
Kutoka WCB mzigo huu ulianza kusikia kwenye masikio ya mashabiki Februari 12, 2021 ukiwa na nyimbo nne.

7. Air Weusi – Weusi (819k)
Hip Hop nayo haikubaki nyuma, wasanii hawa kutoka Arusha walitoa album hiyo Machi 12, 2021 ikiwa na nyimbo 14.

8. New Chui (EP) – Rayvanny (468k)
Hii ni EP yake ya pili baada ya Flower aliyoitoa Februari 2020. New Chui imetoka Oktoba 29 ikiwa na nyimbo sita.

9. Wanibariki (EP) – Nandy (428k)
EP hii yenye nyimbo za injili ilitoka Aprili 20, 2021 ikiwa na nyimbo tano

10. 20 – Lady Jaydee
Album hii ya nne kwake kwenye maisha ya muziki aliitoa kama sehemu ya kusherehekea ukongwe huo ambapo aliiachia Februari 24, 2021.

Kwa ujumla katika mtandao huo album ya bongofleva iliyosikilizwa zaidi ni Afro Beat ya Harmonize (mara milioni 14) iliyotoka Machi 14, 2020 wakati EP ya Zuchu inayofahamika kama ‘I Am Zuchu’ iliyotoka Machi 13 inaongoza kwa kusikilizwa ikiwa imesikilizwa mara milioni 9.8.

Send this to a friend