Zijue faida za mwanaume kuwepo katika chumba cha kujifungilia

0
20

Baadhi ya wataalamu wa afya  na wanasaikolojia wamefafanua faida za wanaume kuwepo pamoja na wenza wao wakati wa kujifuungua kwamba kutaongeza upendo, kuondoa upweke na kutamsaidia mwanamke kisaikolojia kupata faraja ya kupunguza uchungu wa kujifungua.

Pia, wanasema uwepo wa mume utamsaidia  mwanamke  kupata hisia chanya  na kujiona anathaminiwa na kujiamini zaidi kuwa mwenza wake yuko naye katika shida na raha.

Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Shedrack Mwaibambe anasema suala la mimba ni la wote wawili,  na uwepo wa wote katika chumba cha kujifungua utasaidia kuongeza uhusiano zaidi kati ya mume na mke na pia kuondoa hofu endapo kutatokea tatizo mume wake atakuwa pale kutoa taarifa kwa urahisi.

“Hii ni nzuri sana kama kweli unampenda mwenza wako utatamani umsindikize na itaongeza uaminifu, mwanamke anakuwa na imani kuwa hata kama nikichanika vibaya mume wangu yupo ataenda kutoa taarifa,,” amesema.

Send this to a friend