Zijue sababu za gari kutoa moshi mweusi

0
98

Moja ya vitu vinavyochangia gari kutoa hewa chafu inayoleta kero kwenye mazingira ni hitilafu katika mfumo wa mafuta. Iwapo mfumo wa mafuta una matatizo utasababisha gari kutoa moshi wenye gesi zenye sumu kwa afya ya mwanadamu na mazingira kwa ujumla.

Mfumo wa mafuta kwenye gari huanzia kwenye tenki la mafuta unapita kwenye chujio (filter) kwenda kwenye pampu nozzle hadi kuingia ndani ya chumba cha muwako (combustion chamber).

Mfumo wa kuingiza hewa ndani ya injini pia unapokuwa na matatizo utasababisha gari lako kuwa chanzo cha kuchafua mazingira, kwa magari ya kisasa yenyewe yana mfumo wa kielektroniki wenye kazi ya kupima kiwango halisi cha mafuta kulingana na hitaji la injini yako.

Pia mfumo wa uchomaji wa mafuta ndani ya injini ya gari unaweza ukawa chanzo cha gari yako kuchafua mazingira, hii ni kutokana kwamba kuna wakati gari inakuwa haina uwezo wa kuchoma vizuri mafuta ndani ya injini kwa sababu ‘spark plugs’ hazichomi, hivyo kusababisha mafuta yaliyoingia ndani ya chumba cha muwako yatoke bila kuchomwa na kusababisha uchafuzi.