Zimbabwe: Corona ni adhabu kwa Marekani na Ulaya

0
43

Waziri wa Ulinzi wa Zimbabwe amesema kuwa virusi vya Corona ni adhabu kwa Marekani na Ulaya kwa kuiwekea nchi yake vikwazo.

Waziri Oppah Muchinguri amesema kuwa sasa raia wa Marekani na Ulaya wanakaa ndani na uchumi wa nchi zao unaharibika kama walivyouharibu uchumi wa Zimbabwe kwa kuiwekea vikwazo.

“Virusi vya Corona vitamfundisha Rais wa Marekani, Donald Trump kwamba yeye siyo Mungu. Lazima waone athari za Corona na waelewe maumivu ambayo tunayapata,” amesema Muchinguri.

Marekani na Ulaya zimeiwekea vikwazo vya kiuchumi na kusafiri dhidi ya watu na kampuni nchini Zimbabwe kutokana na kile wanachodai ni kuzorota kwa hali ya kidemokrasia, haki za binadamu, pamoja na uhuru wa vyombo vya habari.

Rais Emmerson Mnangagwa ni moja ya watu walioathiriwa na vikwazo vilivyowekwa na Marekani.

Hadi sasa kumeripotiwa jumla visa zaidi ya 167,800 vya Corona duniani kote, lakini hakuna kisa chochote kilichoripotiwa nchini Zimbabwe.

Send this to a friend