Zimbabwe kuwalipa fidia trilioni 8 wazungu walioporwa ardhi

0
30

Serikali ya Zimbabwe inatarajiwa kutumia $3.5 bilioni (TZS 8.1 trilioni) kuwalipa faidi raia wazungu waliopokonywa ardhi na kupewa wazawa wa taifa hilo.

Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa, taifa hilo ambalo limekuwa likisumbuliwabna mdororo wa uchumi litauza bondi pamoja na kuomba msaada kwa wahisani wa kimataifa kupata fedha hizo za kulipa fidia.

Zoezi la kuwapokonya wazungu ardhi lilitendeka chini ya uongozi wa Hayati Rais Robert Mugabe ambapo jumla ya wakulima 4,500 wa kigeni walipokonywa mashamba na yaligawiwa kwa wazawa takribani 300,000, hatua ambayo alisema ilisababishwa na wakoloni kupora ardhi.

Kwa mujibu wa makubaliano yaliyosainiwa na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa wazungu hao watalipwa pia gharama za miundombinu iliyokuwa kwenye mashamba yao.

Rais Mnangagwa amesema hatua hiyo ni historia kubwa katika sekta ya ardhi.

Hata hivyo baadhi ya watu wameonesha kukerwa na uamuzi wa kuwalipa fidia wazungu huku wakihoji kuwa wazungu hao wanaolalamika kuwa waliporwa ardhi, wao waliipata wapi? Kwa sababu ardhi yote ni ya wazawa.

Send this to a friend