Zimbabwe yaruhusu bangi kuuzwa kwenye maduka ya dawa

0
16

Zimbabwe imeruhusu bidhaa za katani na bangi kuuzwa kwa mara ya kwanza kama sehemu ya dawa za ziada zinazotolewa kwa wagonjwa.

Mamlaka ya Kudhibiti Dawa ya Zimbabwe imeruhusu wazalishaji, watengenezaji, waagizaji, wauzaji wote wenye leseni ya bangi na katani wanaouza rejareja au kupeleka nje ya nchi kuomba vibali vya kuuza bidhaa hizo.

Wazazi watelekeza watoto, baba aoa na mama aolewa na mtu mwingine

Mdhibiti ameruhusu maafisa wake kukagua maeneo yote ya uzalishaji na kuwataka waombaji wawasilishe sampuli zote za bidhaa ikiwa ni pamoja na cheti cha utambuzi kutoka maabara iliyoidhinishwa.

Hata hivyo, ameongeza kuwa, tayari ameanza kupokea maombi ya kuidhinishwa kwa bidhaa za katani kutoka kwa wadau wake.

Taifa hilo la Kusini mwa Afrika linatafuta ongezeko la mapato yake kutokana na bangi, huku taratibu likiachana na tumbaku. Uidhinishaji huo utasaidia kuchochea uchumi wa nchi unaokadiriwa kufikia dola bilioni 1.25 kwa mwaka.

Send this to a friend