Zingatia haya unapotaka kununua gauni la harusi

0
70

Wakati wa uchaguzi wa gauni la harusi ni wakati unaopaswa kuwa makini ili kujua ni aina gani ya gauni linaloweza kukupa mwonekano wa kipekee katika siku yako. Kabla ya kuanza kutafuta aina hiyo ya gauni, kuna mambo machache ya kuyaweka akilini;

Panga bajeti
Gauni la harusi linaweza kuwa gharama hivyo ni vema kupanga bajeti yako mapema kabla ya kuanza utafutaji. Pangilia ni kiasi gani cha fedha unachotakiwa kutumia kwenye manunuzi kisha simamia kwenye bajeti yako. Usisahau kuchunguza mabadiliko yoyote ya gharama wakati wa kuweka bajeti yako. Magauni mengi yamekuwa yakihitaji marekebisho fulani hivyo hakikisha unaweka bajeti ya ziada kwa hilo.

Panga tarehe ya mwisho
Ni muhimu kujipa muda kwa ajili ya utafutaji wa gauni la harusi. Ni vema kuanza kufanya manunuzi miezi sita kabla ya tarehe ya harusi, hii itakupa muda mwingi kupata chaguo sahihi pamoja na kufanya mabadiliko yoyote utakayoyahitaji. Kupanga muda pia itakusaidia kuepuka kuchanganyikiwa na kufanya maamuzi yasiyo sahihi dakika za mwisho.

Eneo la Harusi na Majira
Gauni lako la harusi linatakiwa kuendana na eneo pamoja na kipindi cha harusi. Kama utakuwa na harusi ya kanisani utahitaji kuvaa kuendana na sheria za kanisa, endapo harusi yako itafanyika sehemu ya ufukweni itakupasa uvae gauni litakalokufanya kuwa huru.

Ni muhimu pia kuangalia majira ya mwaka ambapo harusi yako itakwenda kufanyika. Nguo ya lesi ya mikono mirefu inaweza isiwe chaguo zuri katika kipindi cha majira ya joto.

Jipime Gauni
Usinunue gauni kisa tu lina muonekano mzuri, hakikisha unajaribu gauni ili kuhakikisha jinsi gani linaonekana kwako. Kila gauni huonekana tofauti kwa kila mtu, hivyo ni muhimu kujua linaonekana vipi kwako. Pia weka akilini kuwa magauni mengi yatahitaji kubadilishwa ili kuendana na kipimo chako halisi

Send this to a friend