Unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza kile ambacho utakizungumza ama utakionesha kwake kinaweza kukuathiri au kikakutafsiri wewe ni mtu wa aina gani.
Zingatia mambo haya 6 yatakayokupa heshima unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza;
1. Kumbuka jina lake
Tafadhali kumbuka jina la mtu unayezungumza naye hasa unapokutana naye mara ya kwanza. Jaribu njia mbili tofauti, moja ni pamoja na kutaja jina lake wakati wa mazungumzo na njia nyingine ni kutaja jina lake wakati mnapoagana.
2. Kuwa msikilizaji mzuri
Ikiwa umekutana naye mtandaoni, tafadhali mpe nafasi ya kuzungumza badala ya kuongea mengi kuhusu wewe. Mara nyingi tunahisi kuna mambo mengi ya kuvutia kuhusu sisi ambayo watu wengine wanapaswa kujua. Kuwa msikilizaji mzuri badala ya mzungumzaji mzuri ikiwa unataka kujenga muunganisho mzuri wa mwanzo katika mkutano wa kwanza.
3. Zingatia mada ya kuzungumza
Jaribu kujadili mada ambayo itampendeza mwenzako zaidi. Ikiwa anazungumza sana juu ya hali ya kiuchumi au mada ambayo inajadiliwa sana kwenye vyombo vya habari, jaribu kujenga mazungumzo juu ya mada hiyo.
4. Zingatia
Kuwa msikilizaji mzuri kunahitaji umzingatie mwenzako. Zingatia lugha ya mwili wako ili kuhakikisha kwamba inaambatana na ujumbe unaokuvutia, na epuka kupiga miayo. Ni vyema pia kutaja kile ambacho mwenzako anazungumza ili kuonesha kwamba unasikiliza na kuelewa kile anachojaribu kuzungumzia.
5.. Mfanye ajisikie wa muhimu
Unaweza kumsifia kwa mambo ambayo anaweza kufanya vizuri zaidi yako hata kama ni vitu vidogo, na uviseme kwa dhati.“ kama ningekuwa wewe nisingeweza kumaliza kazi haraka sana, naweza kuchukua muda mrefu kuliko wewe,” au “ni vigumu sana kwangu kufanya hivyo mara kwa mara,” kwa kufanya hivyo atakuchukulia wewe kama mtu anayethamini juhudi za watu wengine.
6. Tabasamu
Jaribu kuwa na tabasamu zaidi wakati wa mazungumzo. Ikiwa unatabasamu wakati wa mazungumzo, mwenzako pia atafanya jambo lile lile ambalo litaunda muungano bora wa awali.