Zipi sababu za mahakama kutamka kuwa ndoa iliyofungwa ni batili?

0
27

Kutokana na mahakama kutotambua ndoa na kuziita batili baada ya mke au mume kudai mirathi pindi mwenza wake anapofariki, watu wengi hujiuliza kwanini ndoa hizo huitwa batili ilihali wenza hao walifunga ndoa?

Swahili Times tumezungumza na Wakili Benjamin Nyagawa ambaye ameeleza kuwa kuna baadhi ya mambo yanayopelekea ndoa kuitwa batili ikiwemo kufunga ndoa chini ya umri unaotambulika kisheria, kufanya udanganyifu au ikiwa mtu huyo amewahi kufunga ndoa ya kikristo awali.

“Kama mtu ni mkristo ndoa inafungwa ndoa moja tu, kwa maana hakuna ndoa za watu wengi kwenye ukristo, kwahiyo ukifunga ndoa za wake wengi kwenye ukristo moja kwa moja inaweza kuwa batili,” amesema.

Mchungaji aamriwa kumrudishia muumini fedha alizodai ni fungu 10

Ameongeza, Kwa mfano mtu ameoa baadaye wakakorofishana kila mtu akaendelea na maisha yake, kama hawakwenda kuvunja ile ndoa mahakamani au baraza lolote lenye mamlaka ya kuvunja hiyo ndoa maana yake ni kwamba ukifunga ndoa juu ya ndoa inakuwa ni batili.”

Aidha, wakili amesema mahakama inapotambua kuwa ndoa hiyo ni batili, maana yake ni kuwa mdai hahusiki na mali za marehemu vinginevyo mtu huyo akiwa ametajwa kwenye wosia wa marehemu.

Send this to a friend