Zitto Kabwe apata ajali mkoani Kigoma

0
42

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amepata ajali ya gari akiwa njiani akitokea Kata ya Kalya kuelekea Lukoma kwenye kampeni katika Jimbo la Kigoma Kusini leo Jumanne Oktoba 6, 2020.

Zitto alikuwa na watu watano kwenye gari yake na wote wako salama ingawa wamepata majeraha na wanahisi maumivu makali.

Wamepata huduma ya kwanza kwenye eneo la ajali baadaye wamepelekwa Kituo cha Afya cha Kalya kilichopo Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Send this to a friend