Zuchu afunguka kuhusu uhusiano wake na Diamond na kufungiwa kwa Cheche

0
63

Mwanamuziki Zuhura Kopa maarufu kwa jina la sanaa, Zuchu, amesema uhusiano wake na Diamond Platnumz ni wa kikazi tu na hakuna kingine zaidi.

Akifanya mahojiano na Bongo5, Zuchu amesema kwamba, tangu uvumi huo ulipoanza kuenezwa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na bosi wake, kama ingekuwa ni kweli, basi watu wangekuwa wamepata angalua kiashiria kimoja kinachothibitisha hilo.

“Watu wanatengeneza stori ambayo haina muendelezo. Kwa sababu kwa muda ambao wameongea, mpaka leo tungepata hata ushahidi wa kitu. So far boss wangu [Diamond] hajawahi kuni-disrespect.”

Akizungumzia wimbo wake wa Cheche kuondolewa YouTube kwa madai ya kukiuka sheria ya hakimiliki (copyright) Zuchu amesema “nime-panic, roho inaniuma sana, namuachia Mwenyenzi Mungu, huwezi jua anataka kunipa baraka gani.”

Mwanamuziki huyo amesema hajatumia kazi ya mtu mwingine kwenye wimbo huo, na kuwa ni mtu tu kaamua kuufungia, lakini anaamini kwamba YouTube wakikamilisha mapitio ya madai yaliyotolewa utaachiliwa.

Mwanadada huyo yupo chini ya lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz na ametambulika kwenye ulimwengu wa muziki kupitia EP yake ya I Am Zuchu aliyoitoa Aprili mwaka huu.

Send this to a friend