Zuchu apigwa marufuku kufanya muziki Zanzibar kwa miezi sita

0
69

Msanii maarufu wa kizazi kipya Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’ amefungiwa kufanya shughuli zote za sanaa visiwani Zanzibar kwa kipindi cha miezi sita baada ya kukiuka maadili ya Kizanzibar wakati wa tamasha la Fullmoon Kendwa lililofanyika Mkoa wa Kaskazini Unguja Februari 24, mwaka huu.

Hatua hiyo imetangazwa na Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, ambapo katibu mtendaji wa baraza hilo, Omar Abdalla Adam ameeleza kwamba Zuchu alitoa matamshi na kuonyesha ishara mbaya wakati wa tamasha hilo, jambo ambalo lilichukuliwa kama kinyume na mila na desturi za Wazanzibari.

Watu sita wakamatwa kwa tuhuma za mauaji ya Rapa AKA

Aidha, Zuchu ametozwa faini ya TZS milioni 1, nyimbo zake kuzuiwa kuchezwa katika redio na televisheni za Zanzibar kwa kipindi hicho pamoja na kutakiwa kuandika barua ya kuomba msamaha na kuthibitisha kwamba hatarudia kosa hilo wakati wa kipindi cha adhabu yake.

Baraza limebainisha kuwa licha ya Zuchu kutokuwa na usajili Zanzibar, alikuwa akifanya shughuli za sanaa.

Send this to a friend