Zuhura Yunus akieleza alivyopokea uteuzi kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais – Ikulu

0
59

Mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Ikulu nchini Tanzania , Zuhura Yunus amezungumza na BBC na kueleza ni jinsi gani amepokea taarifa ya uteuzi wake.

Kabla ya uteuzi huo bi Zuhura Yunus alikuwa mtayarishaji wa vipindi na mtangazaji wa idhaa ya Kiswahili ya Shirika la utangazaji la Uingereza BBC.

Bi. Zuhura anachukua nafasi yake Bwana Jaffar Haniu ambaye amepangiwa kuchukua majukumu mengine kwa mujibu wa taarifa iliyotiwa saini na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya rais.

Uteuzi wake unakuja miezi kadhaa baada ya kuzindua kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

Chanzo: bbcswahili