Zuma jela kwa kudharau mahakama

0
53

Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amehukumiwa kifungo cha miezi 15 jela baada ya mahakama ya juu nchini humo kumtia hatiani kwa kosa la kudharau amri ya mahakama.

Mahakama ya Katiba imemkutana na hatia ya kudharau amri ya mahakama kwa kutofika mahakamani katika kesi ya rushwa inayomkabili kama alivyotakiwa.

Kufuatia hukumu hiyo, Zuma amepewa siku tano kujisalimisha, vinginevyo amri ya kukamatwa itatolewa.

Zuma alifika mahakamani mara moja tu katika kesi yake inayotambulika kama ‘kukamatwa kwa dola’ kutokana na madai kuwa wafanyabiashara walikula njama kushawishi maamuzi ya sera wakati wa utawala wake, na baada ya hapo, alikataa kwenda.

Zuma alitakiwa kufika mahakamani kujibu kesi hiyo, kushindwa kwake kumepelekea hukumu hiyo ambayo imetolewa na mahakama ikiwa ni kuonesha kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Katika nyakati tofauti amekuwa akidai kuwa mashitaka dhidi yake ni njama za kisiasa.

Send this to a friend