Zumaridi adai kuibiwa milioni 19 baada ya polisi kumtoa ndani kwake

0
24

Mshtakiwa Diana Bundala (40) maarufu kama Mfalme Zumaridi amedai kuwa wakati anakamatwa na askari katika chumba chake,  shilingi milioni 19.5 na simu mbili ziliibiwa baada ya yeye kutolewa nje.

Akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza alipowasilisha utetezi wake katika kesi inayomkabili na wenzake  83, Zumaridi amedai siku ya tukio Februari 26 mwaka huu alivamiwa na askari ambao hawakuvalia sare za polisi kinyume na maelezo yaliyowasilishwa mahakamani.

Mzee atangaza kuwaozesha wake zake kwa mwanaume anayewataka

Amedai askari hao walivamia katika chumba chake kisha kumtoa nje huku wao wakiendelea kukagua chumbani bila yeye kuwepo, hatua iliyosababisha askari hao kuchangia upotevu wa pesa na mali hizo.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Clescensia Mushi anatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu utata huo Novemba 9, 2022 ili kuendelea na ushahidi wa kesi msingi inayomkabili.