Zumaridi apangiwa hakimu mpya

0
109

Monica Ndyekobora, Hakimu aliyekuwa akisikiliza shauri la jinai namba 12/2022 linalomkabili Diana Bundala maarufu kama ‘Mfalme Zumaridi’ na wenzake 83, ameondolewa na badala yake shauri hilo litasikilizwa na Hakimu Mkazi, Clescensia Mushi.

Kesi hiyo imeitwa leo kwa ajili ya kusikiliza hoja kutoka kwa mawakili wa utetezi jambo ambalo halikufanikiwa baada ya Hakimu Mkazi, Clescensia Mushi kupanda mahakamani hapo na kutangaza kwamba shauri hilo limepangwa chini yake kuanzia leo Agosti 1, huku akiitaarifu mahakama kwamba atasikiliza shauri hilo kwa siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 15 mwaka huu.

Vielelezo vya wizi vyaibwa Kituo cha Polisi, Polisi wachangishana kulipa

Bila kutaja sababu za Ndyekobora kuondolewa, Mushi ameagiza upande wa Jamhuri kupeleka mashahidi watatu siku hiyo ili kuendelea na usikilizaji wa ushahidi baada ya shahidi mmoja kati ya 20 wa Jamhuri kumaliza kutoa ushahidi wake chini ya Hakimu Ndyekobora.

Send this to a friend