in , ,

AfDB yatoa trilioni 1.7 kujenga SGR Tanzania-Burundi

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeidhinisha dola milioni 696.41 ( TZS trilioni 1.74) za kufadhili Tanzania na Burundi kujenga reli ya ya kisasa (SGR) yenye urefu wa kilomita 651 ambayo itaunganisha mataifa hayo mawili.

AfDB itaipatia Tanzania dola milioni 597.79 [TZS trilioni 1.5] ikiwa ni mikopo na dhamana, huku Burundi ikipata ruzuku ya dola milioni 98.62 [TZS bilioni 247] ambapo kazi ya ujenzi itagawanywa katika sehemu tatu, ambayo ni Tabora–Kigoma (km 411) na Uvinza–Malagarasi (kilomita 156) kwa upande wa Tanzania na sehemu ya Malagarasi–Musongati (km 84) itajengwa nchini Burundi.

Gharama ya jumla ya mradi huo kwa Tanzania na Burundi inakadiriwa kuwa karibu dola bilioni 3.93 [TZS Trilioni 9.84].

Kenya kuondoa visa 2024 kwa nchi zote duniani

“Kama Mpangaji Mkuu wa Mamlaka ya Awali (IMLA), benki itaunda na kuhamasisha ufadhili wa hadi dola bilioni 3.2 kutoka kwa benki za biashara, taasisi za fedha za maendeleo, mashirika ya mikopo ya nje na wawekezaji wa kitaasisi,” imeeleza taarifa ya AfDB.

Burundi ina rasilimali za madini ya kimkakati kama vile lithiamu na cobalt ambayo yanatarajiwa kuingiza mapato makubwa kwa nchi kupitia njia ya reli hiyo. Pia Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa inachangia asilimia 80 ya biashara ya Burundi ya kuagiza na kuuza nje.

Ruto: Ndani ya miaka 10 Kenya haitotambulika

Hospitali ya Muhimbili yazindua mashine inayotibu magonjwa zaidi ya 10