in , , ,

Programu 5 zitakazokusaidia kupata simu yako iliyopotea

Kupoteza simu inaweza kuwa hali ya kufadhaisha haswa ikiwa ina taarifa nyeti au maelezo binafsi. Kwa bahati nzuri, kuna programu kadhaa zinazopatikana ambazo zinaweza kukusaidia kufuatilia na kupata kifaa chako cha Android kilichopotea au kilichoibwa.

Hizi ni baadhi;

Snuko – Android Anti Theft Security
Snuko ni App inayokuwezesha kuifuatilia simu yako ya android kwa kutumia GPS, Wi-Fi na mnara wa simu inayotumia. Snuko pia inaweza kuizima simu yako pale unapogundua kuwa imeibwa na uwezekano wa kuipata haupo na inaweza kukupa taarifa pale kadi ya simu inapobadilishwa.

Anti Theft Droid
Hii ni programu tumishi inayokuwezesha kufuatilia simu yako pale inapokuwa imepotea au kuibwa. Unapoiweka katika simu yako unakuwa na uwezo wa kuifuatilia kupitia kivinjari cha inatenti kama Mozilla au Google Chrome na inaweza kukutumia barua pepe pale inapotokea kadi ya simu yako kubadilishwa na kuwekwa nyingine. Pia inakuwezesha kuona picha ambazo zimepigwa kwenye simu yako pale unapokuwa umeipoteza.

Mambo 4 ya kuzingatia unapoomba kuongezewa mshahara

Total Equipment Protection App
Hii inafanya kazi kama nyingine zilizotajwa hapo juu ikikuwezesha kujua simu yako iko maeneo gani lakini ikiwa na kitu cha ziada ambacho ni uwezo wa kufuta data zako zote zilizokuwa kwenye simu inapotokea ukashindwa kuipata simu yako.

Cerberus Anti Theft
Cerberus Anti Theft inaweza kutumika kuzilinda simu hadi tano kwa wakati mmoja, pia inakutumia taarifa kupitia ujumbe mfupi ‘SMS’ na inaweza kufuatilia simu yako iko maeneo gani kwa kusikiliza mazungumzo kupitia microphone ya simu yako hata kama aliyeichukua haitumii kupiga simu.

Lost Droid
Lost Droid ni programu tumishi ambayo inakusaidia kuitafuta simu yako iliyopotea kwa kutumia kompyuta yako. Inaweza kukutumia taarifa ya mahali simu yako ilipo kupitia SMS bila kusahau kuizima simu yako kwa kutumia SMS.

Mambo 4 ya kuzingatia unapoomba kuongezwa mshahara kazini

Karia: Zawadi ya milioni 188 ya timu ya U15 itajengea miundombinu