in , ,

TFF: Hakuna fedha za maandalizi zilizotolewa na CAF kwa timu zilizofuzu AFCON

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema hakuna fedha yoyote iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa ajili ya maandalizi ya timu zitakazoshiriki fainali za mataifa Afrika (AFCON) hivyo wananchi wapuze taarifa hizo.

Kauli hiyo imekuja baada ya michango mbalimbali inayoendelea kwa ajili ya kuziunga mkono timu za taifa hususani zilizofuzu michuano hiyo, ambapo baadhi ya wadau wa michezo wamedai timu zote 24 zilizofuzu zimekwishapewa fedha za maandalizi na CAF.

“CAF hutoa zawadi za fedha kwa washindi kuanzia hatua ya 16 bora hadi bingwa wa michuano hiyo mikubwa kuliko yote barani Afrika.

Tayari TFF na wachezaji wa Taifa Stars wameshafanya kikao na kukubaliana kuhusu mgao wa fedha hizo za zawadi kwa kila hatua ambayo timu itafika,” imesema TFF.

Fainali hizo za 34 zitafanyika nchini Ivory Coast kuanzia Januari 13 hadi Februari 11 mwaka huu ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi shiriki.

Mwananchi apigwa risasi akiokota kuni ndani ya hifadhi

Gharama za kuingia Kenya zapanda baada ya Serikali kuondoa visa