in , ,

Wagoma kujiunga kidato cha kwanza kutokana na wahitimu kukosa ajira

Baadhi ya wanafunzi waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa wamegoma kuripoti shuleni kwa kigezo kuwa wenzao waliomaliza kidato cha nne, sita na chuo kikuu wapo mitaani bila ajira.

Wanafunzi hao wamesema hali hiyo imewakatisha tamaa ya kuendelea na masomo ya sekondari badala yake kuamua kutafuta shughuli nyingine za kiuchumi ikiwemo mafunzo ya ufundi.

Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe, mmoja wa wazazi wa watoto ambao hawajaripoti shuleni, mkazi wa Kata ya Turwa wilayani Tarime mkoani Mara, Elizabeth Charles amesema binti yake alikataa kuandikishwa na kutaka apelekwe chuo cha ufundi cherehani kutokana na wahitimu wengi kuwa mitaani bila kazi maalum.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mtanda amesema wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ni 52,784, walioripoti ni 32,212 ambapo wanafunzi wa elimu ya watu wazima ni 503.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Paul Chacha amesema ameanza ziara ya nyumba kwa nyumba kwa wazazi walioshindwa kupeleka watoto wao shuleni tangu shule zilipofunguliwa, na kuagiza vyombo vya ulinzi na usalama kushughulika na wazazi hao mara moja.

Viongozi wakuu China, Poland na Cuba kutembelea Tanzania

Rais Samia: Vijana wanatoroka kujiunga na vikundi vya ugaidi nje ya nchi