in , ,

Ishara 4 kuwa unapaswa kubadili haraka matairi ya gari lako

Kumiliki gari kunarahisisha shughuli za usafiri katika nyakati mbalimbali. Lakini pia unapomiliki gari ni muhimu kufanya uchunguzi wa mara kwa mara wa gari lako ili kugundua endapo kuna tatizo lolote ili kuweza kulitatua kwa haraka.

Wakati wa ukaguzi, unapaswa pia kuangalia matairi ya gari ikiwa yanapaswa kubadilishwa kupitia vidokezo hivi vifuatavyo;

Uvimbe kwenye sehemu ya tairi
Uvimbe hutokea baada ya athari zitokanazo na gari kupitia kwenye mashimo au kukanyaga vitu vigumu vinavyoweza kusababisha tairi kupasuka. Tatizo hili linasababishwa na hewa kuingia kati ya eneo la nje na tabaka la ndani na kusababisha kuwepo kwa kifuko cha hewa ambacho kinasababisha eneo hilo kuwa dhaifu na kuwa rahisi kupasuka.

Mtetemeko kwenye matairi
Hali hii ni ishara ya shida mbalimbali zinazotokea kwenye tairi. Shida moja kubwa inayosababisha tairi kuwa na mtetemeko ni wakati mikanda au kamba za ndani zinajitenga kati yake na tairi au kuhama kabisa. Ukiona yanatetema wakati unaendesha gari, unatakiwa kuyabadilisha haraka iwezekanavyo ili kuepuka matatizo makubwa.

Umri wa tairi
Umri wa tairi unaathiri kwa kiasi kikubwa matumizi ya gari kwani tairi likitumika kwa muda mrefu zaidi ya ilivyoelekezwa na watengenezaji ni hatari kwa uhai wako pamoja na gari.

Watengenezaji wanashauri matairi ya gari yabadilishwe ndani ya miaka mitano mpaka sita bila kujali hali ya tairi.

Kuisha kwa kashata (tread)
Kashata (tread) ni moja kati ya vitu muhimu vinavyokuonyesha kwamba matairi ya gari lako yametumika kwa muda mrefu na yanahitaji kubadilishwa. Kimo cha kashata kinakuonyesha kuwa matairi uliyonayo yametumika kwa muda mrefu na unahitaji kuweka mengine.

Dkt. Mpango: Serikali inatarajia kupokea ndege mpya mbili

Waziri Mkuu wa Ethiopia kufanya ziara ya kitaifa ya siku tatu Tanzania