in ,

Polisi kufanya msako wa magari yaliyofungwa ving’ora na yaliyoongezwa taa

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ramadhani Ng’anzi ameagiza kikosi cha usalama barabarani kukamata magari yote yaliyofungwa ving’ora na vimulimuli kinyume na utaratibu.

Akizungumza na vyombo vya habari Ng’anzi amesema magari ya dharura pekee ikiwemo, magari ya Zimamoto, magari ya polisi na magari yanayoongoza misafara ya viongozi ndiyo yanayoruhusiwa kufungwa ving’ora, kinyume na hapo yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua kali ikiwemo faini na kifungo.

Uganda: Mahakama yatoa adhabu kwa wanawake wanaotuma watoto kuomba mtaani

“Nawaagiza ma-RTO wote, wakuu wa usalama barabarani wa mikoa, wakuu wa usalama wa wilaya na vikosi vyote vya polisi kuyakamata na kuyazuia magari yote ambayo yamefungwa ving’ora na vimulimuli kinyume cha utaratibu, na baada ya hapo huyo mmiliki na dereva wa gari apelekwe polisi ashitakiwe, na kabla hajaachiwa gari lake, ahakikishe kwamba limeng’olewa kimulimuli hicho,” ameagiza.

Aidha, jeshi la Polisi limetoa onyo kwa wamiliki wa magari wanaoongeza taa zenye mwanga mkali na kufunga stika kwenye taa za gari likiwataka kuziondoa haraka vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Uganda: Mahakama yatoa adhabu kwa wanawake wanaotuma watoto kuomba mtaani

Mahakama Kenya yaamuru wafungwa kupewa haki ya kuzika wanafamilia wao