in , ,

Uganda: Mahakama yatoa adhabu kwa wanawake wanaotuma watoto kuomba mtaani

Mahakama nchini Uganda imewahukumu zaidi ya wanawake 100 kufanya kazi za jamii bila malipo kwa mwezi mmoja kwa kukiri kuwatumia watoto wao kuomba katika mji mkuu wa Kampala.

Kwa mujibu wa Daily Monitor mahakama pia imepiga marufuku wanawake hao kurejea mjini na kuamuru warudishwe katika wilaya yao ya Napak, Kaskazini mwa Uganda, ikiamuru kuwa iwapo watashindwa kutumikia adhabu yao, watalazimika kutumikia kifungo cha mwezi mmoja jela.

Hata hivyo wanawake hao wameiomba mahakama kuwahurumia kwa kuwa baadhi yao ni wajane na wengine wakisema ni mama wasio na wenza.

Nchi 10 za Afrika zenye kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira mwaka 2024

“Nimesikiliza kilio chao, na kuwahukumu [jela] haitakuwa sawa. Ni lazima nitekeleze adhabu ya kuzuia, nitawahukumu kufanya kazi za kijamii bila malipo, amesema hakimu wa mahakama hiyo, Edgar Karakire.

Kutuma watoto kuomba ni kinyume na sheria za ulinzi wa watoto za Uganda na adhabu yake ni kifungo cha miezi sita jela.

Bashungwa aagiza mkandarasi aondolewe kwa kukosa vigezo

Polisi kufanya msako wa magari yaliyofungwa ving’ora na yaliyoongezwa taa