in ,

Mkurugenzi wa Sumbawanga aunganishwa kesi ya uhujumu uchumi

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewaunganisha washitakiwa wengine saba akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi, Catherine Mashalla katika kesi ya uhujumu uchumi na kufanya idadi ya washitakiwa katika kesi hiyo kufikia 14.

Kesi hiyo imesomwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rebeca Mwalusako huku upande wa Jamhuri ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU, ambapo kwa mara ya kwanza ilitajwa mahakamani hapo Agosti 22, 2023 ikiwakabili washtakiwa saba.

Mashalla ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, ameunganishwa katika shauri hilo namba 5 la mwaka 2023 na kusomewa mashtaka 153, ikiwemo utakatishaji wa fedha, kuunda genge la uhalifu na kughushi malipo kwa njia ya mtandao kinyume na utaratibu.

Mhasibu Wilaya ya Same miaka 20 jela kwa kuhujumu uchumi

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa vile mahakama hiyo haina mamlaka ya kuendesha kesi za uhujumu uchumi.

Aidha, kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 28, mwaka huu ambapo itatajwa tena.

Tanzania yapokea trilioni 1.4 kukabiliana na Malaria, TB na UKIMWI

Serikali yatumia bilioni 2.4 kugharamia timu za Taifa