in , ,

Serikali kufanya maboresho ya sheria ya kampuni ili kuvutia wawekezaji

Serikali imepanga kufanya maboresho kwenye sheria ya Kampuni Sura ya 212 na Sura 213 ya Majina ya Kampuni ili kukuza na kuvutia uwekezaji zaidi nchini na kuendana na mabadiliko ya teknolojia kufuatia maoni ya wadau yaliyodai kuwa sheria hiyo haiendani na mazingira ya sasa ya biashara nchini.

Maoni hayo yaliyotolewa kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) mara baada ya kupokelewa na kufanyiwa utafiti, BRELA ilibaini dosari kwenye sheria hiyo ikiwemo masharti kuwa; ili upate jina la biashara lazima kampuni iwe na watu 20 na iwe na majukumu tofauti manne, ambapo wadau wamependekeza idadi ipungue na kampuni iwe na kazi moja.

BRELA imewasilisha maoni hayo kwa Tume ya Marekebisho ya Sheria Tanzania ambayo inayapitia na kutoa mapendekezo kwa ajili ya maboresho ya sheria hiyo.

Akizungumza Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria nchini, Nathaniel Mandepo amesema maboresho yatakayofanyika ni katika kutengeneza mazingira ya uwekezaji nchini.

“Hatua hizi za awali za kukusanya maoni ya wataalamu itafuatana na utafiti wa mapungufu kwenye sheria, sera na mfumo unaotumia sheria husika kupata taarifa muhimu zitakazosaidia maboresho,” ameeleza.

Akifungua kikao cha mjadala wa mabadiliko ya sheria jijini Dar es Salaam akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), William Erio amesema maboresho ya sheria yanalenga kuwapa fursa wafanyabiashara nchini kuchangamkia masoko ndani ya nje ya nchi.

Tanzania na Rwanda kuboresha ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam

Rais Samia: Sina kundi katika kufanya uteuzi wa viongozi