in , ,

Ufanisi wa Bandari ya Mtwara waongezeka zaidi ya mara mbili

Katika juhudi za kuboresha huduma za Bandari ya Mtwara, mitambo mpya inayojulikana kama harbour crane ya kupakia na kushusha shehena kwenye meli, imewasili bandarini hapo ikiwa na lengo kuongeza ufanisi na utendaji wa bandari hiyo.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Nicodemus Mushi amesema kabla ya uwekezaji huo, Bandari ya Mtwara ilikuwa na uwezo wa kuhudumia takribani tani 400,000 za shehena kwa mwaka lakini baada ya uwekezaji huo, uwezo wa bandari hiyo umeongezeka maradufu na kufikia zaidi ya tani milioni 1 kwa mwaka.

“Uwekezaji huu ulihitaji vifaa vya kisasa ili kuhakikisha kazi inafanyika kwa ufanisi, hivyo tumehamisha vifaa kutoka bandari zingine kama Tanga na Dar es Salaam ili kuhakikisha Bandari ya Mtwara inaboresha utendaji wake na kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi kwa mwaka mzima,” amesema Mushi.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara, Duncan Kazibure, ameelezea matarajio ya kuongezeka kwa ufanisi kutokana na ujio wa mitambo hiyo mpya akisisitiza kuwa mitambo hiyo itachangia sana katika kupunguza muda wa meli kukaa katika gati, huku ikiboresha huduma za usafirishaji.

Takwimu zinaonesha kuwa mwaka 203/24 hadi Januari mwaka huu, bandari ya Mtwara imehudumia zaidi ya tani milioni 1 za shehena, ikionesha ongezeko kubwa ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Rais Samia: Sina kundi katika kufanya uteuzi wa viongozi

Benki ya NMB yaimarisha mfumo wake kuongeza tija katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu