in ,

Wanafunzi wafukuzwa kwa kuiba viti vya shule na kuviuza

Wanafunzi watano wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Chuno, Manispaa ya Mtwara-Mikindani mkoani Mtwara wamefukuzwa shule kwa kuiba viti vya shule na kwenda kuviuza kama vyuma chakavu, Machi 7 mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Shule, Hamisi Kaoneka wakati wa kikao cha Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara na viongozi wa elimu ngazi za shule za msingi na sekondari, watendaji wa mitaa na kata, maofisa elimu na baadhi ya wakuu wa idara wa manispaa hiyo kujadili mustakabali wa sekta ya elimu.

“Tukaenda mpaka kwenye eneo ambalo wanauza chuma chakavu ni maeneo ya Chuno uwanjani pale, kufika pale bahati nzuri ule muda nafika pale ndiyo walikuwa wanapakia kwenye lori,” ameeleza.

Ameongeza kuwa wanafunzi hao sio mara ya kwanza kukabiliwa na kesi ya wizi, kwani walishawahi kushtakiwa shuleni kwa kuiba mabati mtaani na kwenda kuyauza kama chuma chakavu.

Tazama tahasusi (combination) mpya za kidato cha tano zitakazoanza kutumika Julai

Facebook na Instagram kuanza kuwalipa watengeneza maudhui Kenya