in ,

Tahadhari za kuchukua wakati wa kimbunga

Kimbunga ni dhoruba kali inayoanza juu ya bahari katika maeneo ya tropiki yenye upepo wenye kasi zaidi.

Tanzania ilishuhudia kimbunga cha mwisho mwaka 1952 ambacho kilitua mkoani Lindi katika pwani ya Kusini ya nchi.

Hivi karibuni, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari juu ya kimbunga Hidaya katika Pwani ya Bahari ya Hindi huku ikiwataka wananchi katika baadhi ya maeneo kuchukua tahadhari.

Hizi ni tahadhari za kuchukua kujikinga na athari za kimbunga;

  1. Sikiliza vyombo vya habari ambavyo hutoa tahadhari za hali ya hewa. Hii itakusaidia kupata taarifa za hali ya hewa na kuchukua tahadhari za kimbunga.
  2. Pasha wengine habari kuhusu tahadhari za kimbunga. Hii itasaidia kusambaza habari sahihi na kuzuia uvumi ambao unaweza kusababisha hofu isiyo ya lazima.
  3. Amini na kuzingatia taarifa rasmi zinazotolewa na mamlaka husika. Epuka kuamini uvumi au taarifa zisizo rasmi.
  4. Endelea na shughuli zako za kawaida lakini uwe macho kwa tahadhari zitakazotolewa na mamlaka. Kimbunga kinaweza kutokea wakati wowote, hivyo ni muhimu kuendelea kusikiliza na kufuatilia taarifa za hali ya hewa.
  5. Toka maeneo ya chini kando ya pwani. Ikiwa eneo lako lipo chini au karibu na pwani, jitayarishe kuondoka mapema na kwenda maeneo ya juu au maeneo salama.
  6. Kama unaishi katika nyumba imara, funga madirisha na milango ili kuzuia uharibifu. Hakikisha una chakula cha ziada na maji.

Wakati wa kimbunga kikali;

  1. Pakia mahitaji muhimu ya kudumu kwa siku kadhaa. Haya yanaweza kujumuisha dawa, chakula maalum kwa watoto au wazee, na vifaa vingine muhimu.
  2. Iwapo nyumba yako si imara, nenda kwenye eneo la hifadhi au vituo vya vilivyotolewa kwenye eneo lako kulingana na maelekezo ya mamlaka.
  3. Usiwe na wasiwasi kuhusu mali zako, usalama wa maisha yako na familia yako ni muhimu zaidi kuliko mali.
  4. Epuka safari zisizo za ulazima na badala yake utulie nyumbani na familia yako mpaka kitakapokwisha.
  5. Epuka kukaa au kusimama kwenye miti au nguzo za umeme wakati wa kimbunga kwani miti inaweza kuanguka na kuleta athari.
  6. Endelea kubaki kwenye kituo cha hifadhi hadi upokee maelekezo ya kurudi nyumbani kutoka kwa mamlaka husika.

Barrick Tanzania yashinda tuzo tano za usalama mahali pa kazi

Nafasi 45 za Ajira Serikalini