Bunge lakanusha wabunge kuongezewa mishahara hadi milioni 18

0
42

Bunge la Tanzania limekanusha kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe kwamba wabunge wameongezewa mishahara kutoka shilingi milioni 13 hadi shilingi milioni 18.

Kauli hiyo ilitolewa Machi 22, mwaka huu wakati mwenyekiti huyo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara Mjijini Babati mkoani Manyara na kisha video ya taarifa hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunapenda kuujulisha umma kwamba madai hayo ni uzushi na upotoshaji kwa kuwa hakuna mbunge aliyeongezewa mshahara kama alivyodai. Hivyo tunapenda kuwashauri na kuwasihi wananchi kupuuza madai hayo ambayo lengo lake ni kuleta taharuki na kuwagombanisha wananchi na wawakilishi wao,” imeeleza taarifa.

Mkurugenzi wa Sumbawanga aunganishwa kesi ya uhujumu uchumi

Aidha, taarifa hiyo imeongeza kuwa nyongeza ya mshahara ni suala linalozingatia bajeti, na kwamba hakuna utaratibu wa aina yoyote kama huo ambao umetumika kuwaongezea wabunge mishahara.

Send this to a friend