Facebook na Instagram kuanza kuwalipa watengeneza maudhui Kenya

0
67

Wabunifu wa maudhui nchini Kenya watapata pesa kutokana na machapisho yao kwenye majukwaa ya Meta kama vile Facebook na Instagram kuanziaJuni mwaka huu kufuatia makubaliano kati ya Rais William Ruto na rais wa masuala ya kimataifa wa kampuni hiyo Nick Clegg.

Katika taarifa iliyotolewa baada ya mkutano katika Ikulu ya Nairobi, huduma ya vyombo vya habari vya Rais wa Kenya ilisema kuwa maendeleo hayo ni matokeo ya juhudi za serikali za mwaka mzima za kuwawezesha wabunifu kupata mapato kutokana na maudhui yao mtandaoni kama wanavyofanya kwenye majukwaa mengine kama vile YouTube na X.

Kwa upande wake, Rais Ruto amepongeza hatua hiyo akibainisha kuwa itafungua fursa mpya za kuwaingizia kipato vijana wa Kenya, huku akitoa wito kwa Meta kuunganisha malipo kwa M-Pesa.

Programu 5 zitakazokusaidia kupata simu yako iliyopotea

“Sasa waundaji wa maudhui wanaweza kuanza kupata mapato kutokana na mawazo na ubunifu wao. Tunatumia nafasi ya kidijitali kuunda nafasi za kazi kwa mamilioni ya vijana wasio na kazi nchini mwetu,” amesema.

Send this to a friend