Maandamano ya CHADEMA yamezuia jeshi kushiriki usafi

0
37

Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kuonekana akishiriki zoezi la usafi bila vyombo vya ulinzi na usalama kama ilivyoelezwa awali, amesema sababu za kutoshiriki kufanya usafi ni kutokana na Jeshi la Polisi kutoa kibali cha maandamano kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Januari 13 mwaka huu Chalamila alitangaza kuwa Januari 24 vyombo hivyo vitashiriki kikamilifu usafi katika maeneo ya mkoa wa Dar es Salaam Januari 23 na 24, 2024.

Chalamila amesema baada ya kibali kilichotolewa na Jeshi la Polisi waliona si sawa kwa vyombo hivyo kuendelea na zoezi hilo na badala yake kukipa nafasi chama hicho kufanya maandamano yao.

Wagoma kujiunga kidato cha kwanza kutokana na wahitimu kukosa ajira

“Tumewaacha wafanye kwanza ili wasije wakasema demokrasia yao ya maandamano ilizuiliwa. Kwanini tumefanya hivyo, kwenye sheria kuna vifungu vinasema unapompa kwa mkono huu halafu unamnyang’anya kwa mkono huu sio sawa.

Hivyo, tuliona kama maandamano yameruhusiwa polisi huwezi tena kuwapeleka barabarani,” amesema.

CHADEMA wanaandamana mkoani Dar es Salaam ili kupinga kuwasilishwa kwa miswada mitatu ya Sheria za Uchaguzi bungeni pamoja na kupanda kwa gharama za maisha nchini.

Send this to a friend