Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru wafungwa wote nchini humo kupewa haki kama binadamu wengine, ikiwemo haki ya kuhudhuria mazishi ya wanafamilia wao, isipokuwa kama kuna sababu za msingi za kukataa kutoa ruhusa.
Uamuzi huo ni kufuatia kesi iliyowasilishwa na mwanahabari wa zamani, Moses Dola ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela mwaka 2018 kwa mauaji ya mke wake.
Polisi kufanya msako wa magari yaliyofungwa ving’ora na yaliyoongezwa taa
Baadaye, mwanaume huyo aliwasilisha ombi la kuhudhuria mazishi ya mama yake na kukataliwa, hatua aliyoiita kuwa ni ukiukaji wa uhuru na kuwashutumu wakuu wa magereza kwa kuwanyima wafungwa haki za kibinadamu.