Shirika la Utafiti wa Anga za Juu (NASA) hivi karibuni limeripoti kuwa Machi mwaka huu hali ya joto kali imeikumba Afrika Mashariki, hali iliyozilazimu serikali kuchukua hatua za dharura ikiwa ni pamoja na kufunga shule nchini Sudan Kusini kwa muda wa wiki mbili.
Aidha, Mataifa matano ya Afrika ikiwemo Afrika Kusini, Gabon, Kenya na Sudan Kusini yaliripotiwa kuvunja rekodi kwa viwango vya juu vya joto.
Pasipoti 10 za nchi za Afrika zenye nguvu zaidi
Yahoo Finance imetoa orodha ya nchi 10 zinazoongoza kwa joto kali zaidi barani Afrika. Orodha hii inajumuisha wastani wa halijoto ya kila mwaka.
- Burkina Faso: 29.3°C
- Mali: 29.2°C
- Senegal: 29.0°C
- Mauritania: 28.9°C
- Benin: 28.7°C
- Gambia: 28.5°C
- Guinea-Bissau: 28.1°C
- Ghana: 27.7°C
- Sudan: 27.6°C
- Niger: 27.6°C
Chanzo: Business Insider Africa