Ndege ya wachezaji yapata hitilafu angani wakielekea AFCON

0
24

Ndege iliyokuwa imebeba timu ya taifa ya Gambia kuelekea kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) imelazimika kutua kwa dharura baada ya kupata hitilafu kwenye mfumo wa usambazaji wa hewa ya oksijeni.

Ndege hiyo iliyokodiwa kuelekea Ivory Coast imelazimika kurejea kwenye mji mkuu wa Gambia, Banjul, dakika 10 baada ya kuruka, ambapo marubani waligundua mfumo wa kusambaza oksijeni umepata hitilafu.

Kamati ya Waamuzi: Kona waliyopata Simba dhidi ya Singida FG ni batili

Kocha wa timu hiyo, Tom Saintfiet, amesema wachezaji na benchi la ufundi wamenusurika kifo kwa sababu walikuwa wakivuta hewa hatari ya Carbon monoxide kutokana na hitilafu iliyotokea.

Kampuni inayoendesha chombo hicho ya Air Cote d’Ivoire imesema inafanya uchunguzi kubaini chanzo cha hitilafu hiyo.

Send this to a friend